Somo la Kwanza:Mwa 12:1-4a
Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na
jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami
nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe
uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio,
naye akulaaniye nitamlaani; na
katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. Basi Abramu akaenda, kama Bwana
alivyomwamuru;
Wimbo wa Katikati: Zab 33:4-5, 18-20, 22
Kwa kuwa neno la Bwana lina adili, Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu. Huzipenda haki na hukumu, Nchi
imejaa fadhili za Bwana.
Somo la Pili:2 Tim 1:8b-10
Uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri
ya nguvu ya Mungu; ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri
ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake.
Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele, na sasa inadhihirishwa kwa
kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima
na kutokuharibika, kwa ile Injili;
Injili:Mt 17:1-9
Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye,
akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani; akageuka sura yake mbele yao; uso wake
ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru. Na tazama, wakatokewa na
Musa na Eliya, wakizungumza naye. Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni
vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako
wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. Alipokuwa katika kusema, tazama,
wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu,
ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.
Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana. Yesu
akaja, akawagusa, akasema, Inukeni, wala msiogope. Wakainua macho yao, wasione
mtu ila Yesu peke yake. Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza,
akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu
atakapofufuka katika wafu.
No comments:
Post a Comment