MATENDO YA FURAHA
(Jumatatu na Jumamosi)
Tendo
la kwanza;
Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama
wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
Tendo la pili;
Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti.
Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
Tendo la tatu;
Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
Tendo la nne;
Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
Tendo la tano;
Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe
Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
M
MATENDO YA UCHUNGU
(Jumanne na Ijumaa)
Tendo la kwanza;
Yesu anatoka jasho
la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko
la dhambi.
Tendo la pili;
Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie kuacha
dhambi za uchafu.
Tendo la tatu;
Yesu anatiwa miiba
kichwani kwa ajili
yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda
kiburi.
Tendo la nne;
Yesu anachukua Msalaba
kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
MATENDO YA UTUKUFU
(Jumatano na Jumapili)
Tendo la kwanza;
Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
Tendo la pili;
Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
Tendo la tatu;
Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la nne;
Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
Tendo la tano;
Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
MATENDO YA MWANGA
(Alhamisi)
Tendo la kwanza;
Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
Tendo la pili;
Yesu anageuza maji
kuwa divai huko
Kana. Tumwombe Mungu atujalie
kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
Tendo la tatu;
Yesu anatangaza Ufalme
wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme
wake kwa toba ya kweli.
Tendo la nne;
Yesu anageuka sura.
Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
Tendo la tano;
Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka
kwa ajili ya wengine.
LITANIA YA BIKIRA MARIA
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumie
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utusikie
Kristo utusikilize
Mungu Baba wa Mbinguni,…… Utuhurumie
Mungu Mwana Mkombozi wa dunia ……… Utuhurumie
Mungu Roho Mtakatifu.................... Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu
Mmoja...................... Utuhurumie
Maria Mtakatifu..................... utuombee
Mzazi Mtakatifu wa Mungu..................... utuombee
Bikira Mtakatifu Mkuu wa Mabikira...................... utuombee
Mama wa Kristo..................... utuombee
Mama wa Neema ya Mungu.............................. utuombee
Mama Mtakatifu sana....................... utuombee
Mama mwenye usafi wa Moyo........................... utuombee
Mama mwenye ubikira......................... utuombee
Mama usiye na doa......................... utuombee
Mama mpendelevu....................... utuombee
Mama mstajabivu....................... utuombee
Mama wa Muumba...................... utuombee
Mama wa Mkombozi........................... utuombee
Mama wa Kanisa....................... utuombee
Bikira mwenye utaratibu............................. utuombee
Bikira mwenye heshima............................. utuombee
Bikira mwenye sifa............................ utuombee
Bikira mwenye uwezo............................ utuombee
Bikra mweye huruma............................. utuombee
Bikra mwaminifu…...................... utuombee
Kioo cha haki.......................... utuombee
Kikao cha hekima............................ utuombee
Sababu ya furaha yetu.............................. utuombee
Chombo cha neema............................. utuombee
Chombo cha kuheshimiwa.............................. utuombee
Chombo bora cha ibada.............................. utuombee
Waridi lenye fumbo........................... utuombee
Mnara wa Daudi........................... utuombee
Mnara wa pembe............................ utuombee
Nyumba ya dhahabu............................. utuombee
Sanduku la Agano............................ utuombee
Mlango wa Mbingu........................... utuombee
Nyota ya asubuhi............................ utuombee
Afya ya wagonjwa............................ utuombee
Kimbilio la wakosefu....................... utuombee
Mtuliza wenye huzuni............................ utuombee
Msaada wa waKristo............................. utuombee
Malkia wa Malaika........................... utuombee
Malkia wa Mababu........................... utuombee
Malkia wa Manabii........................... utuombee
Malkia wa Mitume........................... utuombee
Malkia wa Mashahidi............................ utuombee
Malkia wa Waungama dini............................. utuombee
Malkia wa Mabikira........................... utuombee
Malkia wa Watakatifu wote............................. utuombee
Malkia uliyepalizwa Mbinguni............................ utuombee
Malkia wa Rozari takatifu............................. utuombee
Malkia wa amani........................... utuombee
Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,… Utusamehe ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye
dhambi za dunia,… Utusikilize ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye
dhambi za dunia,… Utuhurumie.
Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,............Tujaliwe ahadi za
Kristo.
Tuombe
Ee Bwana Mungu,
utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili
siku zote; na kwa maombezi matukufu ya Maria
Mtakaatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate
na furaha za milele.
Kwa Kristo Bwana wetu,
Amina.
No comments:
Post a Comment