Lisikieni neno la Bwana, enyi waamuzi wa Sodoma; tegeni
masikio msikie sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora. Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe
mbele za macho yangu; achene kutenda mabaya; jifunzeni kutenda mema; takeni
hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni
mjane. Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana.
Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.
Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.
Wimbo wa Katikati:Zab 50:8-9, 16-17, 21, 23
Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako, Na kafara zako ziko mbele yangu daima.
Sitatwaa ng’ombe
katika nyumba yako, Wala beberu katika mazizi yako.
Injili:Mt 23:1-12
Yesu aliwaambia makutano na wanafunzi wake, akasema,
Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yoyote
watakayowaambia, myashike, na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao,
msitende; maana wao hunena lakini hawatendi. Wao hufunga mizigo mizito na
kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao. Tena
matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupapanua hirizi
zao, huongeza matamvua yao; hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi
mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi. Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi
nyote ni ndugu. Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye
wa mbinguni. Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye
Kristo. Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. Na yeyote atakayejikweza
atadhiliwa; na yeyote atakayejidhili atakwezwa.
No comments:
Post a Comment