Somo la Kwanza: Yer 18:18-20
Waliposema, Njoni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana
sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno
halitampotea nabii. Njoni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno
yake yoyote. Niangalie, Ee Bwana, ukasikilize sauti ya wanaoshindana nami. Je!
Mabaya
yalipwe badala ya mema? Maana wameichimbia nafsi yangu shimo. Kumbuka jinsi
nilivyosimama mbele zako, ili nisema mema kwa ajili yao, nikaigeuze ghadhabu
yako isiwapate.
Wimbo wa Katikati: Zab 31:4-5, 13-15
Injili: Mt 20:17-28
Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalemu aliwachukua wale
wanafunzi kumi na wawili faraghani; na njiani akawaambia, Angalieni, tunapanda
kwenda Yerusalemu; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa wakuu wa makuhani na
waandishi nao watamhukumu afe; kisha watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki,
na kumpiga mijeledi na kumsulibisha; na siku ya tatu atafufuka. Ndipo mama yao
wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno.
Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi
mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.
Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe
nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza. Akawaambia, Hakika mtakinywa kikombe
change; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri
kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu. Na wale kumi
waliposikia, waliwakasirikia wale ndugu wawili. Lakini Yesu akawaita, akasema,
Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao
huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu yeyote anayetaka kuwa
mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu yeyote anayetaka kuwa wa kwanza
kwenu na awe mtumwa wenu; kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali
kutumikia na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
No comments:
Post a Comment