Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili 15/3/2020

SOMO 1:Kut. 17:3 – 7

Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung’unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu? Musa akamlilia Bwana, akisema, Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe.

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumamosi 14/3/2020

SOMO 1: Mik. 7:14-15, 18-20

Walishe watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, wakaao peke yao, mwituni katikati ya Karmeli; na walishe katika Bashani na Gileadi, kama siku za kale. Kama katika siku zile za kutoka kwako katika nchi ya Misri nitamwonyesha mambo ya ajabu.
Ni nani aliye Mungu kama wewe,

Tafakari ya Neno la Mungu, Ijumaa 13/3/2020

SOMO 1: Mwa. 37:3-4, 12-13, 17-28

Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee wake, akamfanyia kanzu ndefu. Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia, na hawakuweza kusema naye kwa amani.
Ndugu zake wakaenda kuchunga kondoo za baba yao huko Shekemu.

Tafakari ya Neno la Mungu, Alhamisi 12/3/2020

Somo la Kwanza:Yer. 17:5-10

Bwana asema hivi: Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake, na moyoni mwake amemwacha Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, hataona yatakapotokea mema; bali atakaa jangwani palipo na ukame, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.